“WACHANENI NA SIZE 8 HAKUNA ASIYEKOSA HISTORIA” MSANII WA INJILI SHARIFF J ASEMA.

Msanii wa nyimbo za injilii Shariff J anayebobea na wimbo wake mpya unaojulikana kama msaada wa jesu ambao ukitasfiriwa kutoka lugha ya kigiriama wamaanisha msaada wa yesu amewakosoa watu ambao wanaomrushia size 8 cheche za matusi baada yake kuonekana juzi akimwombea mshirika wa kanisa lake.

Chanzo cha matusi haya kimetokana na kuwa picha za size 8 ambaye zamani alikuwa msanii wa nyimbo za secular zimekuwa zikisambazwa mitandaoni ambapo size 8 anaonekana akisakata desi na shabiki na nguo fupi jambo ambalo watu wamekiri kwamba hafai kuwa akihubiri kwani amefanya dhambi nyingi hapo zamani.

msimamo wa sharif kahindi

Shariff amewakosoa watu hawa kwenye mtandao wa kijamii wa facebook akiwaelezea kuwa kumkejeli kupitia historia yake ni vibaya kwani kila mtu ambaye ameokoka ashawai fanya dhambi .Hivyo basi hawafai kumhukumu na picha hizo kwani kama wimbo wake wa msaada wa jeso unaenda sambamba na mwelekeo amabao size 8 aliuchukua na kumkubali yesu na hivi sasa ni bishop mwenye hadhi ya kumwombea na kumtakasa mtu yeyote .

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started