Bingwa na ustaadh Wa Nyimbo Za Injili Max Ngala ameuzindua Wimbo mpya ambao ni WA pili Toka mwezi wa Aprili kungoa nanga .Max ametia bidii iliopita ya mchwa akihakikisha kuwa mashabiki wake wanashiba kimziki na pia Kiroho.
Max Ngala ambaye ametajwa na mchapishaji Mashuhuri wa Nyimbo PrestaBlogs kama msanii wa wikii anaendelea kun’gaa Kwenye uwanja wa Injili akiwa msanii amabaye Kwa Sasa ananyimbo mingi huu mwaka akiwapita mabingwa na mababe waliotajika Kwa Kina na upana.

Wimbo Mpya wa max Ngala aliouwachilia katikati mwa wiki ni wimbo ambao Max anatoa ushuda Kwa Mambo amabayo amepitia akimtolea maulana shukran Kwa Kuwa kama si yeye angekuwa ameshambulia patupu, aendeleza na kutangaza kuwa maishani mwake ni mungu tu ambaye humskiza , humkosoa na pia humrekebisha Kwa huruma anapo potoka na hivi anasababu mingi Sana za kumshukuru ibadan katan.
Utazame Wimbo mpya Wa Max Ngala Wewe Ni Mungu Hapa ;
https://youtu.be/w7OIKgcrb5o

