Mwimbaji marufu Isaka Makaya ameuwachilia mzuka wake mpya unaoitwa Azimio ambao unampigia Kiongozi wa upinzani raila odinga ambaye anawania kiti cha raisi kwenye uchaguzi mkuu utakao fanyika mwezi ujao tarehe tisa Agosti.
Isaka Makaya alizaliwa mwaka wa 1976 katika jimbo la migori na eneo alikozaliwa kulikuwa na wasanii mashuhuri kama Collela Mazee, prince jully na wengineo na hapa ndipo alipata motisha wa kuwa msanii tajika.
Hivi sasa makaya anafahamika kwa uwezo wake ustaadh katika kucheza ala za mziki kama Bads , drum, guitar na pia kwenye uimbaji na hivi ni vipaji zinaweza onekana kwenye wimbo wake mpya Azimio Raila Baba .
Azimio Baba Ni Wimbo unaomfuata Makaya ambaye ni shabiki mkuu wa raila akimpa sifa na pongezi kinara huyo wa chama cha odm pamoja na martha karua ambaye ni mgombea mwenza akiwasafia kwa utenda kazi wao hapo awali akiwaombea dua njema katika safari yao ya kuelekea ikulu kuu mnamo Agosti.

